Jumanne , 18th Mar , 2025

Jeshi la Israel linasema kuwa linafanya mashambulizi makubwa katika Ukanda wa Gaza, huku wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas ikiripoti kuwa zaidi ya Wapalestina 400 wameuawa

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema linashambulia kile lilichokiita maeneo ya ugaidi ya Hamas.

Mashambulizi yanaendelea na IDF hivi karibuni ilitoa maagizo mapya ya kuhama kwa maeneo mengi.

Mahmoud Abu Wafah, naibu waziri wa mambo ya ndani huko Gaza na afisa wa ngazi ya juu wa usalama wa Hamas katika eneo hilo ni miongoni mwa waliofariki.

Hili ni wimbi kubwa zaidi la mashambulizi ya anga huko Gaza tangu kusitishwa kwa mapigano kuanza tarehe 19 Januari.

Mazungumzo ya kuongeza muda wa usitishaji mapigano Gaza yameshindwa kufikia makubaliano