Jumanne , 18th Mar , 2025

Mtayarishaji wa muziki wa miondoko mipya alimaarufu Bongo fleva S2kizzy ameamua kujimwagia maua yeye mwenyewe kabla ya wengine kummwagia sifa mtayarishaji huyo.

Pichani N S2kizzy Diamond na Rayvanny

S2kizzy ameandika ujumbe katika mtandao wa Instagram akidai kuwa yeye ndio mtayarishaji bora zaidi wa muziki kwa Afrika Mashariki kwa waandaaji wote waliohai na waliofariki hakuna kama yeye tangu muziki uanze kwa upande wa Afrika Mashariki, Ameeleza hayo baada ya wimbo ambao ameutayarisha wa Msanii Rayvanny NesaNesa Kufanya vizuri katika mataifa yaliyo nje ya Afrika.

 

S2kizzy katika mtandao wa instagram ameandika.... ''SIJAWAHI KUONA KAMA MIMI,HAKUNA PRODUCER ALOWAHI KUFANYA GLOBAL HITS AND INTERNATIONAL PENETRATION SONGS KAMA MIMI … DEAD OR ALIVE , NOBODY NOBODY NOBODY IN ALL GENERATIONS SINCE MUZIKI UANZE EAST AFRICA . Sio KENYA Sio UGANDA Sio BURUNDI Sio RWANDA Sio TANZANIA

I’m HIM …. !!! TUMEWAPA INGINE HIYO #NESANESA Big S/o To Rayvanny na Diamond FOR ALWAYS DELIVERING Blessings To My beats''