Jumatatu , 29th Dec , 2025

Tukio hilo limetokea kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, hali iliyosababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Kifusi cha matope kimeporomoka na kuziba sehemu ya barabara kuu ya Morogoro–Iringa katika eneo la Iyovi, Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro kuathiri matumizi ya barabara hiyo.

Tukio hilo limetokea kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, hali iliyosababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amefika katika eneo hilo na kuona uhalisia wake na ametoa wito kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara hiyo kuchukua tahadhari wakati huu wa mvua ili kuepusha madhara zaidi.