
mwanamuziki wa miondoko ya Jazz Uganda Isaiah Katumwa
Aidha Isaiah ameelezea kuwa pamoja na burudani hiyo itakayofanyika mwezi oktoba mwaka huu, amesema kuwa wanatarajia kufanya harambee hiyo chini ya taasisi iliyoanzishwa na mwanamuziki Philly Bongoley Lutaaya iliyobatizwa jina Philly Lutaaya Cares (PLC).
Aidha mtoto wa gwiji huyo Tezra Lutaaya, ambaye ni mwanzilishi wa wa taasisi hiyo ameelezea kuwa mapato yatakayopatikana kupitia shindano hilo yatapelekwa kwa ajili ya kuanzisha chuo cha ufundi huko Kinoni, Gomba kwa ajili ya kutoa fursa kwa wanawake wajane na vijana.
