Ijumaa , 19th Jul , 2019

Msanii na Mwanasiasa katika ngazi ya ubunge wa jimbo la Starehe nchini Kenya Charles Njagua maarufu kama Jaguar, ameonekana kutembelea nchini Tanzania katika miji ya Dodoma na Dar Es Salaam.

Jaguar

Jaguar ameonekana hivyo kupitia picha aliyopost katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kuandika "Habari za asubuhi kutokea Dar Es Salaam".

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

...Good morning from Dar es Salaam.

A post shared by Hon. Jaguar (@jaguarkenya) on

Jaguar kwa sasa yupo nje kwa dhamana baada ya kusota jela kwa wiki kadhaa zilizopita, kwa kosa la kutoa lugha za kichochezi , na maneno ya chuki kwa wageni na watanzania ambao wanaishi nchini Kenya.

Aidha baada ya kutoa kauli hizo na kuwekwa jela, Jaguar mwenyewe amekuwa akikataa kwa kusema watu hawakumuelewa vizuri na wala hakuwa na nia ya kuwafukuza wageni na wala hana shida yoyote na watanzania waishio nchini Kenya.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

.....

A post shared by Hon. Jaguar (@jaguarkenya) on