Picha ya pamoja Harmonize na Kajala
Harmonize ametoa ujumbe huo kwenda kwa Kajala kwa njia ya maandishi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo ameeleza kuwa
"Kuwa makini na watu wanaokufuata kipindi una matatizo na mtu fulani wengine walijibanza wakisubiri inyeshe, mchawi harogi bila sababu kwa sasa huwezi kuona kundi hilo la watu ila ukitizama nyuso zao na maneno ya kashfa, ukiwa timamu utanielewa Mungu akusimamie life time partner".
Pia tayari msanii Harmonize ameachia wimbo mpya ambao unamlenga mpenzi wake huyo wa zamani juu ya kuachana kwao huku amemuomba isiwe vita na waachane kwa amani.
Zaidi tazama hapa chini kwenye video.