
Kulia ni picha ya Hayati Magufuli, kushoto ni tattoo aliyoichora Harmonize
Tattoo hiyo ameichora kwenye mguu wake wa kulia akiwa Lagos nchini Nigeria, kisha ameandika maneno yafuatayo "Mimi nime-sacrifice maisha yangu kwa ajili ya watanzania maskini".
Picha na video hizo akiwa anachora tattoo hizo amezishea kwenye 'Insta Story' ya ukurasa wake wa Instagram halafu mwisho wa picha hizo akaandika 'RIP Kamanda'.