
Picha ya Msanii Gigy Money
Gigy amethibitisha hilo kupitia instagram yake kwa kuandika ‘’tumefunguliwa’’ baada ya BASATA Januari 5, mwaka huu kupitia kwa Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza, Matiko Mniko,kutangaza kumfungia kutojihusisha na shughuli za Sanaa baada ya msanii Gigy kutumbuiza jukwaani akiwa amevalia nguo zilizodhalilisha utu wake na kubugudhi hadhira ya wapenda sanaa.
Tukio hilo lilitokea akiwa katika tamasha la muziki huko jijini Dodoma katika uwanja wa Jamhuri.