![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2025/02/18/vx.jpg?itok=vSXCF64D×tamp=1739879677)
Wachezaji Kibu Denis (Simba) na Aziz Ki (Yanga)
Yanga walishuka dimbani dhidi ya Singida Black Stars hapo jana, jambo lililoibua maswali ni kikosi cha Singida BS kilichoanza. Katika kikosi hicho wachezaji muhimu wa kikosi hicho kama Arthur Bada, Jonathan Sowah, Ibrahim Imoro na Beki Antony Trab wote wakianzia benchi.
Mjadala juu ya ukaribu wa wamiliki wa Klabu ya Singida BS na Yanga ndio uliochochea zaidi na kuonyesha dhahiri huenda kukawa na upangaji wa matokeo katika mchezo huo, madai mabayo hayajathibitishwa.
Mchambuzi wa Michezo na mtangazaji wa kipindi cha Kipenga Xtra Ibrahim Kasuga akichambua mchezo huo amesema "Simba wakishinda wanaambiwa wamebebwa na waamuzi na Yanga wakishinda ni familia na wamepanga matokeo, Mawazo ya upangaji wa Matokeo zinatokana na viongozi wetu ambao tayari wametujenga katika msingi huo"
Yanga wnaongoza Ligi wakiwa na alama 52 alama 5 mbele ya watani wao Simba wenye alama 47 wakifuatiwa na Azam FC wenye alama 42