
Sasa baada ya kutoka Grok 1 na 2 Dunia imekaa mkao wa kuisubiria Grok 3 ambayo kwa mujibu wa Elon anaitaja kuwa Akili unde bora Duniani
Akili unde ya Elon Musk inayofahamika kama ''Grok A.I'' ni akili unde mahususi kwa ajili ya kukusaidi vitu vidogo vidogo kama vile kujibu maswali, kutatua changamoto na kufikiria kuhusu jambo fulani. Lakini akili unde hii inapatikana kwa watumiaji wa mtandao wa ''X'' ambayo zamani ilikuwa inafahamika kama Twitter.
Kupitia mtandao wake wa ''X'' Elon anaandika Grok 3 kuachiwa usiku wa Jumatatu saa mbili usiku kwa saa za pacific ikiambatana na onesho la kwanza la mfano, Itakuwa akili unde bora Duniani (Kwa hapa kwetu itakuwa siku ya kesho asubuhi na mapema)
Ni kweli ''Grok 3'' anaweza kuwa mpinzani rasmi wa DeepSeek?