Alhamisi , 20th Feb , 2025

Mwanasheria wa zamania wa Klabu ya Yanga, Simon Patrick amesema Yanga na Simba zimekuwa na nguvu kubwa katika soka la Tanzania kuliko mamlaka ya Soka.

Simon Patrick - Aliyekuwa Mwanasheria wa Klabu ya Yanga

Kupitia mtandao wa Instagram ameandika malezo hayo kutokana na mwenendo wa matukio mbalimbali yanayoendelea kwenye mpira wa Tanzania kwa sasa.

''Yanga na Simba zina nguvu kuliko mamlaka za soka nchini. Wasimamizi wa soka letu wako tayari kuzibeba hizi timu kuliko kutenda haki

Pia, Simon amegusia kuhsu mjadawa wa waamuzi kufanya makosa yanayojirudia katika michezo mbalimbali huku kukiibua dalili za upangaji wa matokeo.

"Waamuzi hawafanyi makosa kwa bahati mbaya bali wanatekeleza maelekezo waliyopewa. Muda umefika wa kuvunjwa kwa Kamati ya Waamuzi Tanzania pamoja na waamuzi wote, kwani hawana mchango wala msaada wowote katika maendeleo ya soka la nchi yetu.''-Simon Patrick Mwanasheria wa zamani Yanga SC