
Hayo ya yamejiri kufuatia utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) Jijini hapo ambapo majirani hao Johanes Johnbosco na Yassin Suleiman walitofautiana kwenye matumizi ya ardhi.
Imeelezwa kwamba Johanes aliingia makubaliano ya kuchimba na kujenga shimo la maji taka katika eneo la jirani yake huyo kupitia kwa mmiliki wa awali wa eneo hilo baada ya Johanes kukumbana na changamoto ya mwamba katika eneo lake.
Hata hivyo shimo hilo limekuwa likitumiwa kwa pamoja na mmiliki wa awali hadi mmiliki wa sasa kabla ya kupishana na kumtaka Johanes kuacha kutumia shimo hilo
Baada ya wanasheria hao kufika eneo la tukio wamefikia maridhiano kuwa kwa sasa waendelee kutumia pamoja huku Yassin akitoa kipande cha ardhi yake kumpatia Johanes ili ndani ya miaka mitatu ajenge shimo lake katika kipande hicho.
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid) inaendelea katika Halmashauri zote nane za Jiji la Mwanza ambapo wataalamu wa sheria wanaendelea kutoa elimu na kutatua migogoro mbalimbali.