Jumatatu , 15th Dec , 2014

Katika kuelekea mwisho wa mwaka, Msani mkali wa michano FID Q ametoa mtazamo wake kuhusiana na gemu ya muziki na kusema kuwa, hatua ambazo muziki umepiga mpaka sasa ni nzuri.

msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini Fid Q

Fid Q ameelezea huku wakiwa kama wasanii wakubwa wamejaribu kuweka mfumo sawa kwa ajili ya kunufaisha zaidi vizazi vya baadae.

Staa huyu wa rap, amesema kuwa, kwa sasa bado mapambano yanaendelea kuboresha soko na pia mfumo wa mauzo ya muziki, kutokana na hali halisi kutokuwa katika ngazi ya kumfaidisha msanii.

FID Q pia amewataka mashabiki wake kujua kuwa kwa sasa yupo chimbo akitayarisha video yake ya Bongo HIP HOP kama zawadi ya Krimasi ama Mwaka Mpya.