Jumanne , 9th Mei , 2017

Mfalme wa hip hop anayewakilisha jiji la Mwanza Farid Kuband 'Fid Q' ameweka bayana katu hajawahi kufikiria kama anaweza kuja kufanya kazi na msanii mwenzake Rado ambaye aliwahi kumchana kupitia wimbo wake wa 'usiulize'

Fid Q amezungumza hayo wakati akipiga Story na Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kwamba katu hawezi kusema kama ipo siku ataweza kufanya kazi na Rado kwani historia inaonyesha kwamba mtu wa karibu anaweza kumfanyia kitu kibaya ambacho mtu hawezi kutegemea.

Aidha Fid Q amefunguka kuwa wimbo aliochanwa na Rado wakati mwingine ulikuwa ukitumika kama silaha za kumfukuza sehemu za starehe.

"Mimi nilikuwa msanii ambaye sichanikagi, lakini Rado aliweza kunichana vizuri na wimbo wake ulikuwa hit song kitu ambacho siyo kibaya. Ma Dj ambao tulikuwa hatuivi walikuwa wanatumia ngoma hiyo kama njia ya kunifukuza katika maeneo ya starehe, lakini namkumbuka Rado kwa heshima kabisa kama msanii mkubwa mwenye uwezo wa ki-hip hop na hata game bado linamwitaji" - Fid Q

Hata hivyo Rado aliwahi kufunguka kwamba "Nimewadiss jamaa makusudi kwani nina sababu za msingi za kufanya hivi, sababu ya kumdiss Fid Q ni kwa sababu anajifanya anawakilisha Hip Hop wakati ameniibia mistari yangu na kuitumia katika wimbo wake wa ‘mwanza mwanza’ nayo ni ‘sio kila ndio ina undio kiundani ndio bali kuna baadhi ya ndio zimeambatana na utani’-  Kauli ya Rado baada ya kuulizwa sababu za kumchana Fid Q wakati alikuwa mshkaji wake

Pamoja na kwamba Fid Q amekanusha kuwepo kwa tofauti kati yake na Rado amedai kwa sasa amezima data na haitaji kujua alipo msanii huyo wala kujua anafanya nini, Msikilize Fid Q hapa chini.