Ijumaa , 15th Aug , 2014

Rapa Fid Q, ambaye ni moja ya wasanii wakubwa wa Hip Hop hapa Bongo, baada ya kuachia kazi mpya ya Bongo Hip Hop, amezungumzia muziki huu wa Hip Hop kwa sasa hapa Bongo, na kusema kuwa unahitaji kufanyiwa mabadiliko.

msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini Fid Q

Fid Q amesema kuwa, wasanii wengi wa wakati huu wana tatizo la kutokujitambua wenyewe pamoja na kutokupata mafanikio ya kutosha kutoka katika kazi zao, haya yakiwa ni mambo ambayo pia atayadhihirisha kupitia uchambuzi alioufanya katika makala yake ya Bongo Hip Hop aliyoiandaa.