Jumamosi , 7th Mar , 2020

Msanii wa filamu Dorah Official amefunguka issue inayohusu kumuhonga gari aina ya IST mwanaume  kwa kusema hapa mjini hana mpenzi yeyote na hawezi kufanya tendo hilo la kumuhonga mtu yeyote.

Msanii wa filamu Dorah

Dorah amesema mwanaume anayeonekana wakiwa wote kwenye gari hana mahusiano naye na mpenzi wake yupo vijijini, pia haiwezi kutokea kumpa  mtu gari kwa sababu hata yeye bado ana shida nyingi na familia inamtegea.

Akizungumza hayo kwenye show ya eNewz ya East Africa TV, inayoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 12:00  hadi 12:30 jioni Dorah amesema

"Siwezi kumuhonga mtu kwenye maisha yangu, najua nilipotoka, ninapoelekea na ninachokifanya kwanza mama yangu ana mambo mengi yanamzonga na matatizo ya familia yangu yaniumiza kichwa halafu nimuhonge mwanaume IST haiwezi kutokea"  ameeleza Dorah

Aidha Dorah ameongeza kusema "Ninayeonekanaga naye kwenye gari sio mpenzi wangu, kwanza sina mwanaume mjini hapa mimi mwanaume wangu yupo vijijini huko mkoani Iringa, na anaumia akisikia hizi taarifa za kashfa kama nimemhonga mtu gari"