Ijumaa , 14th Feb , 2014

Kundi la muziki wa mwambao, Dar Modern Taarab ambao wamerudi na nguvu mpya pamoja na mabadiliko kadhaa ikiwepo kuongeza wanamuziki wapya ndani yake, katika siku hii ya wapendanao wameamua kuwapatia mashabiki wao zawadi ya Albam mbili, Kitwitwi na Oh My Honey ambapo usiku wa leo watafanya onyesho kubwa la uzinduzi jijini Dar es Salaam.

Wakiwa wamejipanga vizuri na shughuli hii kubwa, kutoka katika kundi hili, kwa niaba ya wenzao, Bi Mwanahawa Ally, Hassan Vocha na Sikudhani Ally, wamewataka mashabiki wao kutokosa tukio hili kubwa ambapo pia wametumia nafasi hii kutoa ujumbe wao wa siku hii ya wapendanao.

Wasanii hawa kwa pamoja wamewataka watu kuzingatia mapenzi katika maisha ya kila siku sambamba na kupenda burudani na kuacha kupoteza muda katika changamoto za kawaida za maisha ya kila siku.