Jumatano , 27th Aug , 2014

Makundi 10 yaliyofanikiwa kutimba katika nusu fainali ya mashindano makubwa ya Dance 100% 2014, leo hii yameweza kufika katika ofisi za EATV kwaajili ya maelekezo na uchaguzi wa nyimbo ambazo watatumia katika mpambano kuelekea fainali.

mashindano ya kucheza muziki nchini Dance100% 2014

Makundi haya wakiwepo Quality Boys, The WT, Dar Crew, Best Boys, The Winners Crew, Wakali Sisi, Tatanisha Dancers, GOP, Wazawa Crew na Mazabe Powder ambao kwa sasa wapo katika maandalizi makali kuwania zawadi ya ushindi, kitita cha shilingi milioni 5.

Makundi haya yatakutana uwanjani katika mpambano wa hatua ya nusu fainali tarehe 13 mwezi Septemba mwaka huu.