Jumatano , 18th Nov , 2015

Hatimaye msanii wa muziki Bobi Wine kutoka Uganda ameachia rasmi rekodi ambayo ameifanya maalum kwa ajili ya kumkaribisha kiongozi mkubwa wa kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, mbele ya ziara yake nchini humo tarehe 27 mwezi huu.

nyota wa muziki wa Uganda Bobi Wine

Rekodi hiyo imepatiwa jina “Welcome Pope Francis” ambayo ameifanya akishirikiana na kwaya ya Rubaga, lengo kubwa likiwa ni kuwatayarisha raia wa Uganda kwa ujio wa kiongozi huyo na pia kuwaandaa waumini wa dini ya kikristo kiroho kwa ajili ya ziara hiyo.

Rekodi hii imetajwa kama wimbo rasmi wa ziara ya papa Uganda, ikiwa imetayarishwa na Tony Houls na Silver Kyagu-lanyi ambapo licha ya kutokuwa na taarifa rasmi, Bobi Wine anatajwa kujivunia kitita kinono cha pesa kutokana na kuhusika kwake katika kazi hii.