Billnass afunguka ukweli kuhusu kumchana Nandy

Jumanne , 13th Apr , 2021

Msanii Billnass amefunguka kusema ana wasiwasi na mashabiki kwamba hawajaelewa kile alichokiimba kwenye wimbo wake mpya wa tatizo ambapo kuna stori inayosemekana amemuimbia Nandy kwa sababu wameachana.

Picha ya pamoja Billnass na Nandy

Akizungumzia hilo kwenye show ya Planet Bongo ya East Africa Radio Billnass amesema 

"Tatizo ni wimbo unaoelezea ukurasa mwingine mpya na stori halisi pia itakuwa project ambayo inamuendelezo, itachukua muda kuielewa kwa sababu inahusiana na maisha yangu ila nina wasi wasi sana watu hawajaelewa vile ambavyo natamani waelewe"

"Ukiisikiliza hii stori na watu ambavyo wanaioanisha ni vitu viwili tofauti, inaweza ikawa inaoana lakini kuna utofauti sana,  ni stori endelevu nitaidadavua vizuri kwa sababu ni stori inayoendelea".

Billnass na Nandy wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu na hadi kufikia hatua ya kuvalishana pete ya uchumba mwaka jana 2020