Alhamisi , 29th Oct , 2015

Staa wa muziki Ben Pol, ametolea ufafanuzi kutoonekana akitoa sapoti kwa wasanii aliowatambulisha katika gemu, akiwepo Alice na pia Heri Muziki, hatua ambayo inayoonesha kuwa star huyo amewaweka kando chipukizi na kuendelea na mishe zake binafsi.

Staa wa muziki nchini Ben Pol

Katika mahojiano na eNewz, Ben ameeleza kuwa hiyo haimaanishi hata kidogo kuwa ameacha kusapoti wasanii wanaochipukia, ambapo anaendelea kufanya hivyo na wasanii wengine kama anavyoeleza hapa.

Kwa upande mwingine, Ben Pol amezungumzia mapokezi ya ngoma yake na Avril – 'Ningefanyaje' ambapo ameweka wazi kuwa anajivunia na kuchana mawimbi kwa kazi yenyewe licha ya kuiachia katika kipindi kigumu cha uchaguzi.