Bebe Cool adokeza juu ya harusi

Jumatano , 9th Jun , 2021

A Living legend Bebe Cool atamani kufunga harusi na mzazi mwenzie Zuena Kirema hii inakuja baada ya kupata ushawishi mkubwa siku ya Jumamosi alipo alikwa kutumbuiza kwenye harusi ya rafiki yake King Ivan Goodheart.

Picha ya pamoja Bebe Cool na Zuena Kirema

Ni muda sasa umepita tangu Bebe amemuahidi mkewe Zuena kufunga nae harusi kubwa na ya kifahari na huwenda ndoto hiyo ya muda mrefu ikatimia baada ya kuonesha shauku kubwa ya kumpa Zuena harusi ya ndoto yake.

Msanii huyo wa Uganda ametumia mtandao wake wa instagram kuelezea hisia zake kwa kusema  "Jumamosi, nilitumbuiza kwenye harusi ya rafiki yangu King Ivan Goodheart na ilinifanya nisisimke zaidi kuhusu siku ya harusi, Mwenyezi Mungu anilinde mimi, mke wangu, familia, na marafiki ili tuweze kuishi na kuona siku hiyo’’.