Jumanne , 16th Jun , 2015

Msanii aliyewahi kutamba kwenye gemu la Bongo fleva mwaka 2004, kwa wimbo wake uitwao nitacheka ambao alimshirikisha Dully Sykes na Mh. Temba sasa amerudi rasmi kwenye gemu upya na wimbo mpya uitwao NACHEKA ambao amewashirikisha

Juma Nature na Mchizi Mox.

Mr Cheka amesema alikuwa kimya baada ya kusafiri nje ya nchi kwa muda mrefu ila sasa amerudi rasmi tena na kuamua kuendeleza muziki maana ni kitu anachokipenda.

"Nilikuwa nje ya nchi kwa muda mrefu ila nilivyofika niliamua kufanya kazi na Juma Nature na pia Mchizi Mox maana ni watu ninaowakubali na niliona kwamba wanafaa katika wimbo huu". Alisema Mr Cheka.

Wimbo huo wa Nacheka wa Mr. Cheka umefanyika Katika studi za Ozz Records zilizoko jijini Dar es salaam na Producer wa wimbo huo anaitwa tsuki (suki).

" Video ya wimbo huu wa nacheka itatoka rasmi tarehe 1 mwezi wa saba, napenda kuwaambia watu kuwa video hii ni moja kati ya video kali sana hivyo watu waisubirie kwa hamu sana. Audio ya wimbo huu unaweza isikiliza kwenye redio mbalimbali hapa nchini na pia kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii" aliongeza Mr. Cheka

Mr Cheka amemalizia kwa kusema kuwa wimbo huu ni kama muendelezo wa wimbo wake wa ntacheka ambao alimshirikisha Dully Sykes na Mh.Temba mwaka 2004 na upo kwenye album ya Mh. Temba iitwayo maskini jeuri, amesema anarudi tena kwenye game kwa staili hii ili kuwakumbusha watu halafu ndio ngoma zingine kali zaidi zitafuata