
Amber Lulu
Amber Lulu ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya "Vunga" aliyomshirikisha producer T-touch, amesema hayo leo kupitia mahojiano na EATV&Radio Digital.
"Kila mtu kaumizwa ila kwa sasa mapenzi hayana nafasi kama kazi yangu, kazi yangu ina nafasi kubwa kuliko haya mapenzi, mtu kukusaliti ndio kunaumiza kuliko kitu chochote, kila mtu niliyekua naye ameshawahi kunisaliti"
Amber lulu amekuwa na mahusiano na rapa Young dee, Barnaba classic, Aslay, Rami gallis na pia aliwahi kuwa na mahusiano na msanii Prezzo kutokea nchini Kenya , ambaye waliachana Julai 2018. Kwasasa kuna fununu kuwa anatoka na Nuh Mziwanda.