Jumatano , 14th Dec , 2016

Kampuni ya burudani ya Afrikasongs.com inayofanya shughuli ya kuuza nyimbo za wasanii kwa njia ya mtandao imefichua siri kwa wasanii wa Tanzania wenye nia ya kutajirika kupitia kazi zao za muziki.

Dully Sykes kwa niaba ya Afrikasongs.com akiwa jukwaani tayari kukabidhi tuzo ya wimbo bora wa mwaka

Mwakilishi wa kampuni hiyo ambayo pia ilikuwa ni moja ya wadhamini wa Tuzo za EATV, Dully Sykes amewashauri wasanii wa Tanzania kuuza kazi zao kupitia kampuni hiyo ili kupata pesa zinazoendana na ubora wa kazi zao kwa kuwa kampuni hiyo  inamlipa msanii asilimia 75 ya mauzo.

Dully amesema kampuni hiyo itaendelea kudhamini tuzo hizo hususani katika kipengele hicho cha wimbo bora wa mwaka, kwa kuwa wanaamini tuzo hizo zitafika mbali, na zitazidi kuwa bora ikizingatiwa pia kuwa EATV inafika mbali na kuwafikia watu wengi barani Afrika.

Pia Dully ambaye alikabidhi tuzo ya wimbo bora wa mwaka, amezungumzia maandalizi na utoaji wa tuzo hizo, huku akitoa maoni yake kuhusu washindi waliopatikana.

Msikilize hapa Dully Sykes......

sauti ya Dully Sykes
Tags: