Ijumaa , 13th Nov , 2015

Nyota wa muziki Afande Sele anajivunia kuwa moja kati ya watu ambao wamewashawishi mheshimiwa Joseph Mbilinyi 'Sugu' na vilevile Joseph Haule 'Prof Jay' kuingia katika siasa na safari zao kufanikiwa.

Nyota wa muziki Afande Sele

Afande Sele ambaye baada ya kutangaza kuachana na muziki na kujihusisha na kilimo, amesema kuwa, kutokana na nafasi hiyo, atatumia urafiki wake na Prof Jay kuyasema yale yote aliyokuwa anataka kuwasemea wana Morogoro Bungeni, kama ambavyo binafsi anaeleza hapa.