Jumanne , 15th Apr , 2014

Msanii wa muziki 2face Idibia ameendelea kuonesha jitihada na mipango mikubwa katika muziki wake, ambapo staa huyu ametangaza ujio wa albam yake mpya kabisa, itakayosimama kwa jina 'Rewind, Select and Update..'

2 Face

Albam hii itaambatana na nyingine za wasanii Dammy Krane na Rocksteady ambao anafanya nao kazi chini ya lebo moja.

2Face amesema kuwa, albam hii mpya mbali na kubeba kazi kadhaa mpya, pia itahusisha ngoma zake kali za zamani ambazo zimefanyiwa remix.

Albam hii inakuja ikifuatia ile ya Away and Beyond ambayo ilitoka mwaka 2012 mwezi Aprili ikiwa na kazi zinazofanya vizuri kwa sasa kama vile Spiritual Healing, Dance Floor na Rainbow.