Alhamisi , 11th Feb , 2016

Zaidi ya nyumba 100 zilizopo mtaa wa Balyehele kata ya Ilemela Jijini Mwanza zimebainika na kujihusisha na wizi wa nishati ya umeme kwa zaidi ya mwaka mmoja na hivyo kulisababishia shirika hilo hasara ya mamilioni ya fedha.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Felchesmi Mramba.

Nyumba hizi zimebainika kuunganishiwa umeme na wateja watatu wa shirika hilo wakati wa msako wa kuwabaini watu wanaojihusisha na wizi wa umeme unaoendeshwa na maafisa wa Tanesco mkoa wa Mwanza.

Akizungumzia tukio hilo Mhandisi wa Tanesco Mkoani humo, King Fokonya wa kitengo cha udhibiti mapato ya shirika hilo jijini Mwanza amesema baadhi ya wananchi wamekuwa na tabia ya kujichukulia maamuzi licha ya kufahamu wanalihujumu shirika hilo huku afisa alama wa shirika hilo John Chirare akitoa onyo wanaojiunganishia umeme kiholela

Kwa upande wake afisa alama wa shirika hilo mkoa wa Mwanza John Chirera amesema wamegundua watu hao watatu kila mmoja amewaunganishia umeme zaidi ya watu 40 hivyo shirika hilo limeamua kusitisha huduma kwa wateja hao pamoja na kukata umeme katika nyumba zote hizo.