Jumamosi , 25th Feb , 2023

Leo ni siku ya uchaguzi mkuu wa urais nchini Nigeria, Idadi kubwa ya watu  zaidi ya milioni 87 ambao wanastahili kupiga kura imejitokeza.

Wengi wao ni vijana, na walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kupanga foleni saa chache kabla ya uchaguzi kufunguliwa saa 02:30 asubuhi saa za nchi hiyo.

Taarifa zinasema  Maafisa wa uchaguzi waliripoti saa kadhaa kuchelewa katika vituo vingi vya kupigia kura, na katika baadhi ya maeneo bado walikua hawajajiokeza.  Pia kumekuwa na ripoti kwamba alama za vidole na teknolojia ya utambuzi wa uso inayotumiwa kuwaidhinisha wapiga kura kuharibika katika baadhi ya maeneo.

Mjini Lagos, ngome ya chama tawala cha APC, kumekuwa na ripoti za ghasia na wizi wa masanduku ya kura. Upigaji kura unatarajiwa kumalizika saa  08:30 mchana  saa za nchi hiyo , ingawa mtu yeyote ambaye amejiunga na foleni kabla ya hapo ataruhusiwa kupiga kura, ambayo inaweza kumaanisha mamilioni ya watu.

Wagombea watatu wanaonekana kuwa mstari wa mbele kumrithi Rais Muhammadu Buhari. Wanaowakilisha vyama viwili vikubwa vya kisiasa ni Bola Tinubu na Atiku Abubakar. Mwingine, Peter Obi, ambaye anaungwa mkono hasa na vijana katika maeneo ya mijini.

Mpaka muda huu Upigaji kura umemalizika rasmi lakini mamilioni ya watu ambao wako kwenye foleni katika vituo vya kupigia kura nchi nzima bado wanaweza kupiga kura. Katika baadhi ya maeneo kusini mwa nchi hiyo, upigaji kura haujaanza.