Jumatano , 15th Jul , 2015

Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, iliyopo Jijini Arusha, imezindua wiki ya Nelson Mandela ambayo kilele chake Julai 18 mwka huu kwa kuwahamasisha vijana wa shule za Sekondari kupenda masomo ya Sayansi ili kuwa na wataalamu wengi

Viongozi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chuo Kikuu cha East China Normal University.

Akizungumza jana jijini Arusha, wakati wa ufunguzi wa sherehe za wiki hiyo, Makamu Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Prof. Burton Mwamila, amesema kila mwaka tangu 2013 huadhimisha maadhimisho hayo kwa kutenga wiki nzima kwa ajili ya kumuenzi Mzee Madiba kwa kuhamasisha uwepo wa Sayansi nchi za Afrika.

Amesema kuwa wanaamini kwa kushirikisha vijana waliopo mashuleni kuipenda sayansi, watafanikisha kuingiza vijana engi katika kupenda masomo ya sayansi na kuyafanyia kazi kwa faida ya taifa na kizazi kijacho.

Prof. Mwamila amesema kuwa mbali na kuhamasisha vijana katika kushiriki wiki hiyo, pia wataendesha kongamano la masuala ya Nishati ili kubadilishana mawazo kwa ajili ya kuleta maendeleo ya uchumi Afrika.

Amesema katika kongamano la Nishati watapata uzoefu kwa wadau wa Sayansi toka nchi ya Afrika Kusini, ambao wamenufaika na Nishati zao, hivyo tunaamini wakibadilishana uzoefu watapata faida kubwa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Ntibenda, amesema wao kama Mkoa wanastahili kuanzisha wiki hiyo, ili kumuenzi mzee Madiba ambaye alitaka Taasisi hiyo ijengwe Tanznai Mkoani Arusha, hivyo kama serikali wataishiriki iki hyo ipasavyo kwa siku zijazo itageuzwa na kuwa shirikishi kwa Mkoa mzima.

Amesema Mzee Nelson Mandela alikuwa mwanaharakati na aliyepigania ubaguzi wa rangi, bado alitamani kuona bara la Afrika linajikwamua na kujitegema katika ubunifu na utumizi wa sayansi na teknolojia.

Ntibenda amesema alifanya jitihada hizo kwa lengo la kuendelea mapambano dhidi ya uhaba wa rasilimali watu katika nyanja za sayansi na teknolojia na kuchochea ubunifu na tafiti mbalimbali katika eneo hilo likiwa ni pamoja na kuuza uchumi wa mwafrika.