
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi
Naibu Waziri huyo amesema hayo wakati akizungumza na watumishi katika Halmashauri mbalimbali za mkoani Pwani nakusema kuwa serikali itaendelea kujali maslahi ya Watumishi wa Umma kwa sababu watumishi ndio injini ya Serikali.
“Ni muda mrefu tumekuwa tukililia haki ya kupandishwa madaraja na kupewa stahili nyingine, Rais wetu ametusikia kwani wote waliostahili kupanda madaraja, wamepanda na wenye madai ya stahili zao mbalimbali wamepatiwa, hivyo hili ni deni na ili kulilipa deni hili tunapaswa kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii na uadilifu,” amesema Ndejembi.
Akizungumzia changamoto zinazojitokeza katika zoezi la upandishwaji wa madaraja kwa watumishi wa umma Mhe. Ndejembi amesema, “Changamoto ya upandishwaji madaraja kwa baadhi ya watumishi ni kupuuza ujazaji wa OPRAS (Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi), hawajazi kwa wakati na wanajaza kwa sababu wanaona ni kigezo tu cha upandaji wa madaraja”.
Sambamba na hilo Mhe. Ndejembi amewataka watumishi wa umma kushiriki katika kutoa elimu kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wanaonufaika na mradi wa kutoa ajira za muda kwani suala hilo ni la watumishi wote.