Watuhumiwa wa ushirikina katika Kijiji cha Nyambogo, mkoani Geita
Maamuzi ya kufukuzwa wanawake hao yalifikiwa baada ya Mtemi na Katibu wa sungusungu kijijini hapo kuitisha mkutano wa hadhara ambapo wanakijiji walipiga kura za kuwatuhumu kujihusisha na imani hizo ambapo Madala Edward alipata kura 8, Kefren Sumuni kura16 na Modesta Edward kura 80.
Watuhumiwa hao wa uchawi wakizungumza na East Africa Television wamesema kuwa wanasikitishwa na kitendo hicho kwani wao hawajihusishi na mambo ya kuwachezea kishirikiana Walimu hali inayopelekea Walimu hao kukimbia Kijiji hicho


