Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu mapambano ya kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino),Said Ndonge akiwa na wajumbe wa kamati hiyo
Wakizungumza shuleni hapo kwa niaba ya wenzao, Agness Robert, Franco John na Samson Charles wamesema kutokana na matukio yanayolikabili taifa kwa sasa ya kuuwawa watu wenye ulemavu wa ngozi, wameona kuna haja ya wao kuimarishiwa ulinzi kwani shule yao haina ulinzi wa kutosha na hata uzio wa shule sio wa kuaminika.
Kwa upande wake, mwalimu Samweli Zebedayo, ambaye ndiye mwangalizi wa watoto hao, amekiri kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na miundombinu ambayo sio rafiki kwa watoto wenye mahitaji maalum, huku akisisitiza kuwa swala la ulinzi bado ni tatizo kutokana na kutokuwa na mlinzi mwenye silaha.
Kaimu afisa elimu maalum wa mji wa Masasi, Fadhili Seif Mimu, alikiri kuwepo kwa changamoto nyingi shuleni hapo ikiwa ni pamoja na swala la kutoimarika ulinzi kwa watoto hao zaidi ya 30 wenye ulemavu wa ngozi na kwamba hakuna mlinzi yeyote mwenye silaha, na swala hilo lipo chini ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ambao ndio wanashughulika.