Vitanda
Marufuku hiyo imetolewa na kamishna wa Elimu Dkt Lyabwene Mtahabwa, na hivyo shule zinazotoa huduma kwa watoto walio katika ngazi hizo wanatakiwa kusitisha huduma hiyo ifikapo mwisho wa muhula wa kwanza wa mwaka 2023.
Kamishna Dkt Mtahabwa amesema kwamba huduma ya bweni kwa watoto huwanyima fursa ya kushikamana na familia na jamii zao, kujenga maadili na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwenye familia zao.