Alhamisi , 2nd Jun , 2022

Utafiti umeeleza kwamba watu ambao hawajaoa ama kuolewa wapo kwenye hatari zaidi ya kufariki dunia kwa magonjwa ya moyo, na kwamba hata ule uwezo wao katika kujisimamia huwa ni mdogo ukilinganisha na watu waliooa ama kuolewa.

Mtu mwenye magonjwa ya moyo

Dk Fabian Kerwagen wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Wurzburg Ujerumani amesema kwamba watu waliooa ama kuolewa wanayonafasi kubwa ya kuishi kutokana na usaidizi wanaoupata kutoka kwa wenzi wao ikiwemo kukumbushwa suala la utumiaji wa dawa kwa wakati.

"Tumegundua kwamba wagonjwa ambao hawajaolewa ama kuoa wanashindwa kuhusiana na jamii ukilinganisha na waliooa ama kuolewa na pia wanakosa uthubutu wa namna ya kukabiliana na magonjwa hayo, bado tunachunguza," amesema Dkt. Kerwagen

Aidha Dkt. Kerwagen amewasisitiza wahudumu wa afya kuwauliza wagonjwa wenye matatizo ya moyo kuhusu hali zao za mahusiano na wahakikishe wanawahamasisha ili wawe na uwezo wa kujisimamia wenyewe.