Jumapili , 10th Apr , 2016

Wasanii wa Filamu nchini kote wametakiwa kutumia mandhari za asili zilizoko katika maeneo ya hifadhi za taifa kwenye shughuli zao za kurekodi filamu badala ya kutumia majengo ya kifahari ili kutangaza utalii kwa kupitia kazi zao.

Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Simon Mwakifamba,

Hayo yameelezwa na Meneja Mawasiliano wa Filamu lilifonyika wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA ,Pascal Shelutete wakati akizungumza katika Tamasha la Chama Wasanii wa filamu jijini Arusha (TDFA) lililofanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid .

Shelutete amesema kuwa Tanapa itatoa ushirikiano kwa wasanii watakaoonyesha nia ya kurekodi filamu zao katika maeneo ya hifadhi ambayo ni salama nay a kuvutia yenye maparomoko ya maji na mandhari za kuvutia ambazo zitasaidia kuhamasisha utalii ambao kwa sasa unaongoza kuchangia pato la taifa.

Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii hao Fredrick Kefas amewataka wasanii kutumia taaluma yao katika kuhimiza utalii wa ndani utakaoliingizia taifa pato kubwa na kuinua uchumi wan chi hivyo kuondokana na utegemezi.

Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Simon Mwakifamba, amewataka Wasanii kutumia vizuri fursa ya maonyesho ya kimataifa ya filamu yanayojulikana kama Tanzanite International Film Festival, yatakayojumuisha wasanii mahiri wa filamu kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani,Asia ,Australia .

Tamasha la Wasanii wa Filamu jijini Arusha lilipambwa na michezo mbali mbali ikiwemo timu ya mpira wa miguu ya wasanii wa Kilimanjaro na Wasanii wa Arusha,timu za mpira wa miguu za mkoani Arusha pamoja na mchezo wa netiboli,Michuano bado inaendelea ambapo mshindi wa kwanza atapata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Manyara na Ngorongoro.