Jumatano , 22nd Mar , 2023

Wanawake wawili wa Kijiji cha Kimana wilayani Kiteto Mkoani Manyara, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kiteto kwa kukutwa na nyara za Serikali, ambazo ni Swala na mtoto wa mnyama aina ya Digidigi ambaye yuko hai

Wanawake hao ni  Veronica Paulo (24) na  Witnes Paulo (20) ambapo Machi 20.2023 wakiwa nyumbani kwao wamedaiwa kukutwa nya nyara hizo za Serikali  wakiwa eneo la Njutaa kata ya Partimbo

Afisa Maliasili Wilaya ta Kiteto, Doris Gama ametaja thamani ya mnyama aliyeuawa aina ya Swala kuwa ni dola za Kimarekani 35 sawa na sh 77,000 elfu za Kitanzania

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara RPC George Katabazi amethibitisha tukio na kudai kuwa upelelezi wa tukio hilo unaendelea #EastAfricaTV