Kiongozi wa UKIP, Nigel Farage akishangilia ushindi.
Katika zoezi hilo la kura ya maoni Jiji la London na nchi ya Scotland wamepiga kura nyingi za kutaka kubakia kwenye Umoja wa Ulaya, ila kura zilizobakia ziliathiriwa na matokeo mabaya katika eneo la kaskazini mwa Uingereza.
Kiongozi wa UKIP, Nigel Farage amepogeza matokeo hayo na kuyaita kuwa ni siku ya uhuru wa mataifa ya UK. Matokeo hayo yameiporomosha thamani ya paundi dhidi ya dola katika kiwango kilichowahi kushuhudiwa mwaka 1985.

