Jumatano , 11th Sep , 2024

Wananchi mkoa wa Dar es Salaam, wameiomba Serikali kuingilia kati kuwadhibiti wauzaji wa bidhaa wanaotumia vipimo kwani wamekuwa wakiwapunja na kupelekea bidhaa wanazonunua kutokizi mahitaji.

Alban Kihulla, Afisa Mtendaji Mkuu WMA.

Hayo yamesemwa na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na kudai kuwa wauza nyama ndio wamekitiri na vitendo hivyo huku hawajui wapi kwa kupeleka malalmiko yao.
"Kiukweli wauza nyama wamezidi utakuta umenunua nyama kilo moja lakini ukiishika ni  nusu na robo inatuumiza sana watu wenye familia natamani Serikali iwadhibiti hawa wauzaji ili sisi wananchi tuweze kupata vipimo vilivyo sahihi", alisema  Aisha Khatib, Mkazi wa Dar es Salaam.

"Kwa mfano mimi naagiza matunda Dodoma nikija kufungua Box yani halifiki vile mimi nilikuwa natarajia, na hapo nalipia mzigo pamoja na hela ya usafirishaji nikiwaza napataje faida inabidi nivikate vidogovidogo ili niopate faida kwahiyo hawa watu inabidi wakaguliwe" alisema Baraka Charles, mkazi wa Dar es Salaam.

"Serikali iwakague hawa wauzaji kwa  maana sisi hatujui, tunauziwa tu lakini wakiwa wanakaguliwa mara kwa mara itasaidia sisi wananchi kupata vipimo halisi", Iddy Ramadhani mkazi wa Dar es Salaam.
"Kwenye mizani ni kama kuna kitu huwa wanawekaga katikati yani unakuta mizan hailingani kabisa inabidi na sisi wananchi tuwe mach tuanze kuwa walinzi wa kitu tunachonunua wenyewe", Ramadhan Rajab, Mkazi wa Dar es Salaam.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini, Alban Kihulla, anaelezea adhabu anayweza kukutana nayo mtu anaechezesha mzani.
"Faini kwa aliechezea mzani au anaekutwa bidhaa yake haijafikia uzito unaostahili anakutana na faini ya Laki moja hadi milioni 20 kwa aliyekubali kosa kwa kosa moja kama  hakukubali kosa itabidi kwenda Mahakamani na akibainika faini laki 3 hadi miliomi 50", Alban Kihulla,  Afisa Mtendaji Mkuu WMA.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa wanapohisi bidhaa waliyonunua haijafikia vipimo .
“Watu wengi wanapenda nyama lakini wengi wana malalamiko kuwa nyama haijafika kipimo halisi kama ambavyo watu wanapoenda kujaza mafuta, Ukihisi mafuta niliyowekewa kwenye hicho kituo hayajafika kwenye geji au umenunua mtungi wa Gesi na matumizi yako ni yaleyale na imewahi kuisha, basi toa taarifa”, Alban Kihulla,  Afisa Mtendaji Mkuu WMA.