Jumatano , 19th Jul , 2023

Wananchi wa Kata ya Kijungu wilayani Kiteto mkoani Manyara, wameanza ujenzi wa nyumba za Askari Polisi katika eneo lao ili kurahisha utendaji kazi wa kukabiliana na vitendo vya uhalifu 

Jengo

Akizungumzia ujenzi huo mmoja wa wananchi hao amesema kuwa nyumba hiyo itakapokamilika itaweza kutumia na familia za Askari sita kwani kwa sasa askari hao wanateseka kwa kulala nyumba moja kama wako bwenini.

"Tuliona hatuna Askari wa kike hapa Kijungu, tukaamua kuanzisha ujenzi wa nyumba ya polisi ili tuletewe watumishi hao tukaona inaweza kuwa msaada kwa kuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu," amesema Tilian Mayaseki mwananchi Kijungu

Aidha wananchi hao wamemuomba mbunge wa Kiteto Edward Ole Lekaita, kuwashika mkono wananchi hao ili ujenzi wa nyumba hiyo uweze kukamilika