Jumanne , 17th Jun , 2014

Serikali ya Tanzania imewataka wananchi kuwafichua watumishi wa umma wanaoshiriki katika vitendo vya kuomba na kupokea rushwa mara wananchi wanapokwenda kupata huduma katika taasisi za umma nchini hususani za elimu na afya.

Waziri wa nchi, ofisi ya rais - utawala bora George Mkuchika.

Akifungua maadhimisho wa juma la utumishi wa umma nchini, Waziri katika ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora, Kaptein Mstaafu George Mkuchika amesema nchi zilizofanikiwa Duniani katika kutokomeza rushwa ni zile ambazo wananchi wake wamekataa kutoa Rushwa na kuwafichua wala rushwa.

Kaptain Mkuchika amesema serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa watumishi wanaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.