Alhamisi , 10th Nov , 2016

Wanafunzi watatu wawili wakiwa wa shule ya msingi na mmoja wa Sekondari wamekufa maji wakati wakiogelea maji katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma Ferdinand Mtui.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kigoma Ferdinand Mtui amewataja wanafunzi hao kuwa ni Omary Ramadhani mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Kipampa na Haina Kalenga mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Livingstone, mwanafunzi mwingine ni Hussein Mushi wa kidato cha nne katika shule ya shule ya Sekondari Lusimbi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Amesema wanafunzi hao walipatwa na mauti baada ya kuzama wakati wakiogelea katika eneo la Lutale katika Ziwa Tanganyika juzi jioni na kwamba miili ya marehemu hao imepatikana na kuhifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Kigoma Maweni.