Jumanne , 11th Aug , 2015

Moto umeteketeza maduka 6 katika soko kuu la mjini Morogoro na kusababisha hasara baada ya bidhaa mbalimbali kuteketea kabisa ambapo wafanyabaishara wakitupia lawama shirika la umeme tanzania Tanesco kutokana na kukatikakatika kwa umeme.

Moto wateketeza maduka sita Mkoani Morogoro

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya mashuhuda na wananchi wamesema moto huo umeanza saa sita usiku huku wakilalamikia kuwa umeme hukatika na kurudi bila utaratibu hali iliosabaisha maduka kuungua moto

Nao wafanyabaishara na wamiliki wa maduka hayo wakizungumza kwa masikitiko wametupia lawama shirika la umeme tanesco kuwasababishia hasara kubwa zaidi ya milion kumi kwa kila duka ambapo wameiomba serikali itende haki ili wafanyabiashara hao walipwe fidia

Kwa upande wake afisa uhusiano wa Tanesco mkoa wa Morogoro Marcia Semfukwe akijibu malalamiko hayo amekiri kuwa moto huo umesababishwa na umeme wa tanesco kutokana na hitilafu lakini wamesema wanamtambua mteja mmoja tu na kwamba wafanyabiashara wengine wamejiunganishia umeme bila kibali.