
Mazishi ya Askofu mkuu balozi Novatus Rugambwa, aliyefariki dunia September 16 mwaka huu mjini Vatican yanafanyika leo katika kanisa kuu la Bikira Maria, huku viongozi mbalimbali wa kidini na serikali wakishiriki.
Misa ya mazishi imeongozwa na askofu mkuu wa Jimbo kuu la Tabora, Kardinali Protase Rugambwa, ambaye amesema kanisa limepoteza mtu muhimu, ambaye ametoa mchango katika maendeleo na na ustawi wa kanisa katoliki.
Amesema kuwa kwa Jimbo katoliki la Bukoba, marehemu balozi Rugambwa amefanya mambo mengi, ambayo yameacha alama kubwa na kudumu kwa kanisa, na kwamba hakuwa na tabia ya kujitangaza kwa mambo aliyokuwa anafanya.
Kardinali Rugambwa amesema kuwa marehemu alitoa mchango kubwa, katika kuhakikisha kanisa la Bikira Maria linajengwa na kuwa katika mwonekano lilionao kwa sasa.