
Aucho akimnyang'anya mpira Mukwala
Baada ya Timu ya Taifa ya Uganda kupata faida ya mkwaju wa penalty dhidi ya Somalia, nyota wa Timu ya Taifa ya Uganda Steven Mukwala ambaye pia ni mchezji wa Simba SC pamoja na Allan Okello kila mmoja alitaka kupiga penalty hiyo.
Suala hilo likaingiliwa kati na Nahodha wa timu hiyo ya Taifa Khalid Aucho ambaye alikuwa mchezaji wa Yanga na sasa Singida BS alimfuata Mukwala akauchukua mpira na kumkabidhi Okello apige penalty hiyo ambayo ilifanikiwa kulenga nyavu akaipatia Uganda bao.
Wadau wa soka wanasema kitendo cha Aucho kumnyang'anya Mukwala mpira na kumpa Okello sio cha kiungwana kwani kwenye mpira kuna kujaribu na bahati hivyo Aucho alipaswa kumuachia Mukwala ule mpira ajaribu