
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Felister Petro umri miaka 42 mkazi wa wilaya ya Maswa amefanyiwa upasuaji kwenye hospitali ya wilaya hiyo na kutoa uvimbe wenye uzito wa kilogramu 6.7 ambao amekaa nao kwa kipindi cha miaka minne na hali hiyo iliyomsababishia maumivu makali.
Mbali na maumivu makali pia alishindwa kupata haki ya ndoa hali iliyopelekea kupata watoto wawili huku matarajio yakiwa kupata zaidi ya watoto wanne.
Upasuaji wa mwanamke huyo umefanyika hospitali ya wilaya ya Maswa kupitia madaktari bingwa walioweka kambi hospitalini hapo na kwa mujibu wa mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt Deogratius Mtaki jumla ya wagonjwa 579 wameona na wengine kufanyiwa upasuaji akiwemo Felister Petro.