Mwonekano wa nje wa vyoo vya shule hiyo
Mwenyekiti wa shule hiyo Said Makua akiongea na #EastAfricaTV ameeleza kuhusiana na shifa hiyo na kueleza kuwa wamejaribu kufanya ukarabati kwa baadhi ya sehemu kuweka nyasi pamoja na kubadilisha masinki ya vyoo lakini bado changamoto ni kubwa.
"Ufa na karo lenyewe lishakatika muda mrefu yaani wamefanya tu kuchukua nyasi na kuhifadhi pale kwenye choo kwa sababu hiko choo tumejaribu kufanya ukarabati wa kubadilisha sinki maana yake sinki zilienda zikaisha kabisa jambo ambalo lilikua hatarishi kwa wanafunzi ambao wanasoma hapa shuleni kwa maana hiyo upungufu wa choo ni mkubwa," amesema Mwenyekiti wa shule hiyo.
Wakiwa wametembelewa na wadau taasisi ya Mama Ongea na Mwanao ambao wamefika kutoa msaada wa viatu, Mwenyekiti wa taasisi hiyo Steve Nyerere ameguswa pia na suala hilo la choo na kutoa mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa choo katika shule hiyo