Alhamisi , 2nd Jun , 2022

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limewakamata watu tisa wakijihusisha  na usafirishaji na uuzaji wa viungo vinavyohisiwa kuwa vya binadamu 

Kamanda wa polisi mkoa Kigoma James Manyama amesema walikamatwa katika Kijiji cha Kanyonza wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma baada ya kuzuia katika kuzuizi cha polisi Kihomoka.

Kamanda Manyama amesema kufuatia mahojiano ya kina na watuhumiwa hao walieleza viungo hivyo kuwa vilikuwa vikisafirishwa kwenda Mwanza kwa mhusika huku wakikiri kuwa viungo hivyo vilifukuliwa katika kaburi la mtu mmoja katika kijiji cha migongo Wilayani Buhigwe mkoani Kigoma