Jumanne , 29th Dec , 2015

Wafanyabiashara zaidi ya 300 walioko katika soko kuu la vyakula wilayani Muheza wameigomea serikali na kutishia kutolipa kodi baada ya kutakiwa kuhama kwenda katika soko la Michungwani.

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua na kuzungumza na wafanyabiashara katika soko la Vyakula Michungwani Wilayani Muheza Mkoa wa Tanga ambalo limekataliwa na baadhi ya wafanyabiashara

Wakiongea baaada ya kuandamana mpaka kwenye ofisi za mkuu wa wilaya hiyo wafanyabishara hao wamesema kuwa hawawezi kuhamia katika soko hilo kwa kuwa lipo umbali mrefu na makazi ya watu hivyo wanashindwa kufanya biashara zao kwa faida.

Wafabiashara hao wengi wakiwa kina mama wameziomba mamlaka husika kuingilia kati kwa kuwa wengine wameshaanza kuuziwa nyumba zao kutokana na mikopo walioyokopa katika kuendeleza biashara zao na kujikwamua kiuchumi.

Akiongea mara baada ya mazungumzo na viongozi wa wafanyabiashara hao mkurugenzi wa manispaa ya wilaya hiyo Bw. Adrian Jungu amewataka wafanyabiashara hao kutii sheria hiyo ili waweze kupanua kwa mujibu wa sheria na kuweza kuitendea haki serikali kwa gharama walizoingia katika ujenzi wa soko hilo jipya.