Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
Akiongea na East Africa Radio Mratibu taifa wa taasisi ya utepe mweupe Tanzania Bi. Rose Mlay amesema bila kuwepo kwa huduma za dharura katika kila kituo cha huduma ya Afya nchini ningumu kukomesha vifo vya mama na mtoto.
Kwa mujibu wa utafiti wa kina wa afya uliofanywa na ofisi ya taifa ya Takwimu Tanzania NBS (Demografic Health Survey 2010) inaeleza kuwa vifo hivyo vya mama na mtoto ni sawa na ndege yenye abiria 168 kuanguka kila siku na abiria wote kufariki.
Kwa kila mwanamke mmoja anayefariki kuna wanawake wengine 30 wanapata matatizo makubwa ikiwemo ulemavu na fistula ikiwa inamaanisha kila siku wanawake 720 wanaathirika tukoana na matatizo ya uzazi

Rose Mlay
Bi. Mlay amesema, huduma za dharua ni pamoja na chumba cha upasuaji chenye vifaa muhimu na vinavyofanya kazi vizuri, wodi ya kulaza kina mama wakati wa uchungu na baada ya kujifungua, mashine ya kumsaidia mtoto mchanga mwenye shida ya kupumua na uwepo wa huduma ya damu salama.
Aidha, Bi Mlay amesema ni lazima vituo vya afya viwe na umeme wa uhakika, maji safi na salama, vyoo salama, huduma ya utakasaji vifaa na uhakika wa rufaa, jenereta na mashine ya kuteketeza makondo.
Bi. Mlay ametoa wito kwa wanajamii na Wabunge na Madiwani kusimamia ongezeko la bajeti ya huduma za uzazi za dharura na kuhakikisha uwepo wa matumizi sahihi ya bajeti hiyo.


